Mrisho Ngassa mchezaji bora yanga kwa mzunguko wa kwanza.
mshambuliaji wa Yanga,Mrisho Khalfan Ngassa amechaguliwa Kuwa mchezaji bora kwa klabu hiyo katika mzunguko wa kwanza.
Ngassa ametangazwa na benchi la ufundi la klabu hiyo ya Jangwani kuwa ndiye mchezaji bora zaidi na kuwazidi nyota wengine Haruna Niyonzima,Ally Mustapha’Barthez’ na Didier Kavumbagu.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wamemaliza mzunguko wa kwanza wakiwa kileleni kwa kuwa na pointi 28 na kuziacha Azam FC,Mbeya City na Simba SC zikibaki vichwa chini.
Wachezaji wengine waliochaguliwa kufanya vizuri zaidi ni beki Mnyarwanda,Mbuyu Twite na Hamis Kiiza raia wa Uganda ambao waling’ara kwa vipindi tofauti.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 alisajiliwa akitokea Simba ambapo usajili wake ulitawaliwa na utata mwingi mpaka kupewa adhabu ya kufungiwa michezo sita ya kwanza ya ligi.
Lakini kiungo huyo aliyesifiwa sana na kocha wake,Ernest Brandts aliporejea kutoka kwenye adhabu hiyo alionyesha kiwango bora huku akifunga goli sita kati ya michezo 7 aliyocheza na kutengeneza nafasi nyingi kwa wenzake.
No comments:
Post a Comment